Wataalamu waanza mafunzo kwa vitendo Muhimbili

Mkuu wa Idara ya Maslahi na Mahusiano Kazini, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Nooran Valli akizungumza na wataalamu wa kada mbalimbali za uendeshaji ambao wamepelekwa MNH kwa ajili kupatiwa mafunzo kwa vitendo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ajira na Mafunzo wa MNH, Bw. Abdallah Kiwanga, Bi. Mwanaidi Omary na Bw. Faraji Abdul Hussein ambao viongozi wa wataalamu hao.

Baadhi ya wataalamu wakimsikiliza, Bi. Nooran Valli wakati akifungua mafunzo hayo leo.

Bi. Mwanaidi Omary akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.

Wataalamu wakifuatilia mkutano wa ufunguzi.


Na John Stephen

Leo wataalamu wa kada mbalimbali waanza mafunzo kwa vitendo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).