Wataalamu wa magonjwa ya macho nchini waanza mafunzo Muhimbili

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Sufian Baruani akizungumza katika mafunzo ya siku tano kuhusu presha ya macho. Mafunzo hayo yamewashirikisha watalaamu kutoka hospitali mbalimbali nchini.

Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo.

Profesa Milka Mafwiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akizungumza na washiriki kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yamefunguliwa na Dkt. Baruani.

Washiriki wakimsikiliza Profesa Mafwiri.

Dkt. Hassan Hassan akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki akifuatilia mafunzo kutoka kwa Dkt. Hassan.

Mshiriki kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Dkt. Annamary Stanislaus akijitambulisha kwa washiriki.

Dkt. Neema Kanyaro wa Muhimbili akifafanua jambo.


Na John Stephen

Wataalamu wa magonjwa ya macho kutoka hospitali mbalimbali nchini wametakiwa kujifunza kwa makini jinsi ya kutoa huduma bora ya presha ya macho kwa wagonjwa wenye tatizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Dkt. Sufuan Baruani wakati akifungua mafunzo ya siku tano kuhusu magonjwa ya presha ya macho.

Mafunzo hayo yanafanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga na yanaudhuriwa na wataalamu kutoka Hospitali ya Benjamini jijini Dodoma, Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Hospitali ya CCBRT na Hospitali ya Muhimbili-Upanga.

Dkt. Baruani aliwataka wataalamu hao kubadilishana uzoefu na kwenda kutoa huduma bora kwa jamii na hasa kushughulia tatizo la presha ya macho ambayo imewakumba watu wengi hivi sasa.

“Jambo kubwa ambalo mnapaswa kulifanya ni kwenda kuwafundisha wenzenu haya mliojifunza hapa. Pia, baada ya mafunzo haya nendeni mkazungumze na viongozi wenu katika sehemu zenu za kazi ili muweke mkakati wa kununua vifaa tiba,” amesema Dkt. Baruani.

Naye Profesa Milka Mafwiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) amewataka wataamu wabobezi kutumia uzoefu wao kuwawezesha washiriki kuwa bora zaidi baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

Profesa Mafwiri amewataka wataalamu waliopo kazini kwa muda mrefu kutafuta majibu kuhusu masuala mbalimbali wanayokutana nayo wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.