Wataalamu wa afya watakiwa kufanya tathmini ya kazi zao

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Bw. Victor Mathias akitoa mada wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika katika Hospitali Taifa Muhimbili-Mloganzila yenye lengo la kuwakumbusha wauguzi umuhimu wa kufanya tathmini ya kazi wanazozifanya kila siku.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bi. Christina Mwandalima akitoa shukrani baada ya huhitimishwa kwa mafunzo.


Na Dorcas David

Wataalamu wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila wametakiwa kufanya tathmini ya kazi zao kwa kuandaa miongozo itakayoonesha hatua za kufuata wakati wa kumuhudumia mgonjwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Aga Khan, Bw. Victor Mathias wakati akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wauguzi na wakunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila namna ya kuandaa miongozo watakayoitumia wakati wa kumuhudumia mgonjwa.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha wataalamu wa afya umuhimu wa kuandaa miongozo katika maeneo yao ya kazi na kufanya kutathmini ya kazi zao kwa kuonesha hatua ambazo watazifuata kabla na baada ya kumuhudumia mgonjwa. 

 “Ili tuweze kufanya tathmini ya kazi zetu, tunapaswa kujenga utamaduni wa kuandika miongozo itakayotusaidia kujua hatua za kuchukua baada ya kumuhudumia mgonjwa,” amesema Bw. Mathias.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma za Ukunga, Afya ya Uzazi Mama na Mtoto Mwandalima amesema mafunzo hayo yatasaidia kuendelea kuboresha utoaji wa huduma, pia watatumia mafunzo hayo kuwajengea uwezo wataalamu wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria.

Jumla ya wataalamu 40 wamenufaika na mafunzo hayo ambayo yametolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Agha Khan.