Wataalam Muhimbili waanza mafunzo ya kugundua mapema saratani ya Ini

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalam wa MNH kuhusu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalam wa mfumo wa chakula na ini kutoka Misri, Afrika Kusini na Ujerumani. Kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Madaktari Bingwa wa Afrika na Mashariki ya Kati wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini (AMAGE), Prof. Mohamed Reda Elwakil. Wataalam hao wameanza kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa MNH jinsi ya kuchunguza na kugundua mapema saratani ya ini, kugundua mapema saratani utumbo na kuanza matibabu mapema.

Baadhi ya wataalam wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini wa MNH wakiwa kwenye mkutano leo kabla ya kuanza kwa mafunzo kuhusu mfumo wa chakula na ini.

Prof. Abdel Meguid Kassem kutoka Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri akimkabidhi zawadi Dkt. Swai. Kushoto ni Prof. Mohamed Reda Elwakil, Mkurugenzi wa Mfuko wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika nchi za Kiafrika (AFTAA), Sherine Adel Emam na kulia ni Dkt. Masolwa Ng’wanasayi na Bi. Asia Kibodya.

Dkt. Swai akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa mfumo wa chakula na ini kutoka MNH, Misri Ujerumani na Afrika Kusini.


Na John Stephen

 Wataalam Muhimbili leo waanza mafunzo kuhusu mfumo wa chakula na ini.