Washauriwa kukabidhiana vifaa tiba baada ya kumaliza zamu

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila , Prof. Lawrence Mseru akiongoza kikao cha Baraza la wafanyakazi MNH -Mloganzila. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Nicholous Mshana, kulia ni Katibu Msaidizi Bi. Neema Njau.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi akiwamo, Mhandisi Mhandisi Veilla Matee wakiwa kwenye kikao cha baraza.


Na Priscus Silayo

Wasimamizi wa majengo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Upanga & Mloganzila wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia makabidhiano ya vifaa tiba mara baada ya atakayekuwa zamu kumaliza zamu zao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru alipokuwa akiongoza kikao cha Baraza la wafanyakazi ambapo wajumbe walisema kuwa Vifaa vinaharibika kutokana na baadhi ya madaktari na wauguzi kutofanya makabidhiano rasmi kila wanapomaliza zamu zao.

Prof. Museru amesema kuwa gharama za vifaa tiba nikubwa hivyo tunapaswa kuvitumia kwa kwa uangalifu ili viendelee kufanya kazi kama ilivyokusudiwa kwa muda mreu.

“Kila anayetumia kifaa anatakiwa kukitumia kwa makini na kuhakikisha anakiacha kikiwa salama mara baada ya kumaliza matumizi  ya kifaa husika, hivyo kila block manager aandae utaratibu wa makabidhiano ya vifaa katika block zao, “ amesema Prof. Museru.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za ufundi MNH Mloganzila, Mhandisi Veilla Matee  amesema kuwa kukiwa na usimamizi mzuri wa vifaa kutaepusha vifaa hivyo kuharibika mara kwa mara.