Wananchi kunufaika na huduma za Afya Sabasaba

Daktari wa Upasuaji mfumo wa mkojo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Abdallah Omari akielezea baadhi ya huduma zinazotolewa katika idara ya urolojia ikiwa ni pamoja na kuondoa tezi dume bila kufanya upasuaji, kuondoa kovu kwenye njia ya mkojo bila upasuaji ,pamoja na huduma ya matibabu ya kuvunja mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo kwa njia ya mawimbi mshituko kwa kitaalam (Extracorporeal shock wave lithotripsy).

Bingwa wa watoto Dkt Aika Shoo kushoto pamoja na Afisa Muuguzi Bi. Neonela Leonard kutoka MNH-Upanga wakielezea huduma zinazotolewa katika idara ya watoto pamoja na namna wanavyookoa maisha ya watoto wanaohitaji uangalizi maalumu(PICU)

Wataalamu wa lishe Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila wakitoa elimu kuhusiana na lishe na mtindo bora wa maisha kwa baadhi ya watu waliotembelea banda hilo

Afisa muuguzi kutoka MNH-Upanga akielezea huduma zinazotolewa katika idara ya magonjwa ya dharura na namna wanavyomsaidia mgonjwa mwenye tatizo la kupumua kwa kutumia kifaa maalumu kitaalam (Bag Mask Valve) ili kumpatia hewa safi ya oksijeni.

Bingwa wa ngozi kutoka MNH-Upanga Dkt. Annete Kisongo akitoa ushauri kwa mgonjwa kuhusiana na magonjwa ya ngozi na huduma zinazotolewa katika idara hiyo ikiwemo upasuaji mdogo,vipimo na matibabu.

Baadhi ya madaktari wa macho Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila) wakiendelea kutoa matibabu kwa baadhi ya wateja waliofika kupatiwa huduma katika banda hilo.

Mtaalamu wa macho kutoka MNH-Upanga akimpatia mteja huduma ya miwani ya kusomea mara baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugundulika na tatizo hilo.

Bingwa wa Macho kutoka MNH-Mloganzila Dkt. Catherine Makunja akimfanyia uchunguzi mteja aliyefika katika banda hilo.

Afisa Muuguzi kutoka MNH-Mloganzila Bw. Jackson Petro akichukua vipimo vya awali kwa mgonjwa ikiwemo kupima uzito na urefu kabla ya kwenda kufanyiwa uchunguzi kwa daktari


Na Dorcas David

Wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila wameendela kutoa elimu na huduma kwa wanachi katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya sabasaba.      

Baadhi ya huduma zinazotolewa ni pamoja na huduma za tiba ya dharura,uchunguzi wa afya ya kinywa na meno,uchunguzi wa macho,uchunguzi wa magonjwa ya ngozi na wataalamu wa lishe bora.

Pamoja na hayo wataalamu hao wanatoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikiinga na ugonjwa wa COVID 19 ikiwemo kuvaa barakoa,kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia kitakasa mikono.