Vunja bei watoa zawadi Mloganzila

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru (katikati) akipokea zawadi ya chupa za chai pamoja na vifaa vya kuhifadhia taka kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja bei Bw. Shija Kamanija, kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt.Julieth Magandi .

Dkt. Julieth Magandi akiambatana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja Bei Bw. Shija Kamanija katika ziara fupi ya kutembelea baadhi ya maeneo ya hospitali mara baada ya kuwasili Hospitali ya Mloganzila.


Na Dorcas David

Kampuni ya vunja bei imekabidhi zawadi kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila pamoja na watumishi kwa lengo la kuwapongeza na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na watumishi wa afya katika kwahudumia wagonjwa.


Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Shija Kamanija amesema zawadi zilizotolewa kwa kwa hospitali ni vifaa vya kuhifadhia taka pamoja na chupa za chai ambazo zitatumika wodini.


“Tunatambua mchango wenu katika jamii hivyo tumeona ni vyema kuwapatia zawadi ikiwa ni ishara ya kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kuhudumia jamii lakini pia kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kupata huduma nzuri, naahidi tutaendelea kushirikiana kadri tutakavyojaliwa”amesema Bw. Kamanija.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameishukuru Kampuni ya Vunja Bei kwa kutoa zawadi na kueleza kuwa zitatumika kama ilivyokusudiwa.