TUGHE yatoa zawadi kwa kina mama Mloganzila.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Redemptha Matindi (aliyevaa nguo ya rangi ya bluu) akiwakaribisha viongozi kutoka TUGHE makao makuu (kamati ya wanawake) ambao wametembelea hospitalini hapo leo.

Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Bi. Jane Mbula (kulia) akizungumza kabla ya kugawa zawadi katika wodi ya kina mama katika Hospitali ya Mloganzila.

Dkt. Stahimili Kalulu kutoka kituo cha Afya Kibaha akimpatia mmoja wa kina mama zawadi kwa lengo la kusheherekea pamoja siku ya wanawake duniani.

Bi. Stella Apolo kutoka TUGHE makao makuu akimpatia mzazi zawadi ya kanga, sabuni na sukari.

Baadhi ya wanawake wa Hospitali ya Mloganzila leo wameungana na wanawake wengine duniani katika kusheherekea siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa imefanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wanawake wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga na Muhimbili-Mloganzila wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.


Na Abubakary Mahamoud Omary

Viongozi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) makao makuu, leo wametembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili -Mloganzila na kuwapatia zawadi mbalimbali wanawake waliojifungua na wale waliolazwa na watoto hospitalini hapo.
Ujumbe wa viongozi hao umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Bi. Jane Mbula ambapo amesema lengo la kutoa zawadi kwa kina mama hao ni kuungana nao katika kusheherekea siku ya wanake duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
 ‘’Tumekuja kuwatembelea kina mama na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo kanga, sabuni na sukari kwani lengo letu ni kugusa jamii na kuhakikisha wanawake waliopo mahospitalini nao wanafurahia siku hii ambayo huadhimishwa mara moja tu kwa mwaka’. amesema Bi Mbula.
Pamoja na mambo mengine kiongozi huyo wa TUGHE ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidi kwakua mwanamke ana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya siku ya mwanamke duniani kwa mwaka 2019 inasema “badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”