MUHIMBILI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEIMOSI KITAIFA, WAFURAHI AHADI YA NYONGEZA YA MISHAHARA.

Wafanyakazi wa Muhimbili (Upanga & Mloganzila) pamoja na wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali katika mkoa wa Dar es salaam wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mh. Amosi Makalla wakati akihutubia katika maadhimisho hayo.

Wafanyakazi wa Muhimbili Upanga & Mloganzila wakiwa katika maandamano ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Wafanyakazi wa Muhimbili -Mloganzila wakiingia katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kushiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo mgeni kimkoa alikua Mkuu wa Mkoa Mh. Amosi Makalla

Wafanyakazi wa Muhimbili-Upanga wakiingia katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kushiriki sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambapo mgeni kimkoa alikua Mkuu wa Mkoa Mh. Amosi Makalla

Baadhi ya wafanyakazi wa MNH-Upanga waliopata zawadi ya ufanyakazi bora wakiwa katika picha ya pamoja.

Baadhi ya wafanyakazi wa MNH-Mloganzila waliopata zawadi ya ufanyakazi bora wakiwa katika picha ya pamoja.


Na Sophia Mtakasimba

Watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) leo wameungana na Wafanyakazi wengine duniani  katika kuadhimisha  ya siku ya Wafanyakazi.

Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma, katika viwanja vya Jamhuri ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na kushiriki katika maadhimisho ya  kitaifa, pia Watumishi wa MNH (Upanga na Mloganzila ) wameshiriki maadhimisho hayo katika ngazi ya Mkoa, ambapo jijini Dar es Salam maadhimisho hayo yamefanyika kwenye  Uwanja wa Uhuru huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa huo Mh. Amos Makalla.

Sambamba na maadhimisho hayo pia wafanyakazi 112 wa Muhimbili Upanga na 36 wa Mloganzila wamepata zawadi ya utumishi hodari kwa mwaka 2021/22 na kila mmoja amekabidhiwa kitita cha TZS 500,000/=

Katika hatua nyingine watumishi wameonyesha kuridhishwa na ahadi ya Rais Mh. Samia Suluhu Hassan ya kupandisha mishahara aliyoitoa Jijini Dodoma.

"Nimefurahi sana kwa kweli Mama ameupiga mwingi, natumaini kufikia mwezi Julai mambo yetu yatakuwa mazuri" alisema mmoja wa watumishi wa Muhimbili ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka huu ilikuwa ni 'Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndio Kilio chetu: Kazi Iendelee'”