Muhimbili yapongezwa utekelezaji miradi ya fedha za UVIKO-19

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akizungumza na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (Hawapo pichani) wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za Uviko- 19

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Fedha za Uviko 19.

Wajumbe wa Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Katibu Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru(Kulia) wakielekea kukagua miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi Muhimbili Mhandisi Gaudence Aksante (Kushoto) akitoa maelezo kwa katibu mkuu kuhusu maendeleo ya mradi mmojawapo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akikagua maendeleo ya ukarabati wa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU)


Na Irene Thomson

   .Yasaini mikataba 57 na Wazabuni

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepongezwa kwa hatua ilizofikia katika utekelezaji wa miradi ya afya kutokana na fedha za UVIK0-19 ambapo hadi sasa imesaini mikataba 57 na wazabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba mbalimbali.

 

Pongezi hizo zimetolewa leo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi alipotembelea MNH ili kukagua utekelezaji wa miradi ya fedha za UVIKO-19 ambapo kiasi cha fedha TZS. 25,540,868,000 Bil. zilizopokelewa hospitalini hapo kwa ajili ya miradi ya MNH na kupewa jukumu la kununua vifaa vya Hospitali za Rufaa za Mkoa Amana, Temeke, Mwananyamala na Tumbi.

 

Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema kati ya fedha hizo, MNH ilipangiwa TZS. 11,876,800,000 Bil. kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kama MRI, CT-Scan, Angio suite, vifaa vya ICU, ujenzi na ukarabati wa idara ya magonjwa ya dharura na kitengo cha dharura kwa kina mama wajawazito, n.k. Hadi sasa MNH imesaini mikataba 16 na wazabuni yenye thamani ya TZS.  11,874,740,103 Bil.

 

Prof. Museru amesema, Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke ilipangiwa TZS. 4,071,470,000 Bil kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura n.k. Hadi sasa Temeke imesaini mikataba 11 na wazabuni yenye thamani ya TZS. 3,559,365,995.84.

 

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Amana ilipangiwa TZS. 4,065,490,000 Bil kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura, n.k. Hadi sasa Amana imesaini mikataba 9 na wazabuni yenye thamani ya TZS. 3,586,829,769 Bil. amesema Prof. Museru.

 

Kwa upande wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mwananyamala, Prof. Museru amesema kuwa ilipangiwa TZS. 1,889,490,000 Bil kwa ajili ununuzi wa Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura, n.k. Hadi sasa Mwananyamala imesaini mikataba 10 na wazabuni yenye thamani ya TZS. 1,708,103,228.20 Bil.

 

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tumbi ilipangiwa TZS. 3,641,554,000 Bil. kwa ajili ununuzi wa CT-Scan, Digital X-Ray, Portbale Utrasound, vifaa vya ICU, radiolojia, vifaa vya idara ya magonjwa ya dharura, n.k. Hadi sasa Tumbi imesaini mikataba 11 na wazabuni yenye thamani ya TZS. 3,530,686,314.96. amesema Prof. Museru.

 

Kutokana na maelezo hayo, Prof. Makubi ameonesha kuridhika na taarifa ya Prof. Museru na kuongeza  hizi ni dalili za moja kwa moja kwamba utekelezaji wa miradi utakamilika ndani ya muda husika ambao ni  Aprili mwaka huu.

 

“Kasi ya utekelezaji wa miradi inaridhisha nina matumaini makubwa kuwa miradi hii itakamilika ndani ya muda tuliojiwekea na hata kama muda utazidi nina imani haitakuwa zaidi ya wiki ya kwanza ya mwezi Mei, hivyo nawapongeza sana kwa hatua hii muhimu” amesema Prof. Makubi.