MUHIMBILI WAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA AFYA

Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Victoria Mlele akimfanyia uchunguzi wa afya Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Tanzania Meja Jenerali George William Ingram mara baada ya kutembelea banda la Muhimbili .

Daktari Bingwa wa mfumo wa njia ya mkojo na uzazi kwa wanaume wa Muhimbili-Mloganzila Dkt.Hamis Isaka akitoa maelezo juu ya matibabu ya ugonjwa wa mawe kwenye figo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Daktari Bingwa wa Macho MNH-Mloganzila Dkt. Catherine Makunja akimpima macho Meja Jenerali George Ingram ambapo pia amepatiwa miwani ya kusomea.

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Tanzania Meja Jenerali George William Ingram akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Muhimbili ( Upanga&Mloganzila) hii leo.


Na Neema Wilson Mwangomo

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga nchini Meja Jenerali George William Ingram ametembelea banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) katika maonyesho ya 44 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba na kupongeza juhudi zinazofanywa na Muhimbili katika utoaji wa huduma za afya.

Meja Jenerali Ingram amesema hatua ya kutoa huduma bila malipo hii ni ya kupongezwa kwani inatoa fursa kwa wananchi kuonwa na wataalam na kupatiwa huduma .

Huduma zinazotolewa katika banda la Muhimbili (Upanga na Mloganzila) ni uchunguzi wa macho, saratani ya matiti pamoja na huduma za dharura ambapo kwa wale wanaobaonika kuwa na matatizo wanapatiwa rufaa kwenda Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kupatiwa matibabu stahiki.