Muhimbili kuongeza vifaa tiba kukidhi mahitaji ya wagonjwa

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila , Prof. Lawrence Mseru akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi, MNH -Upanga. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Adv. Eneza Msuya, kulia ni Katibu Msaidizi Bi. Merina Rwechungura.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka MNH-Upanga wakiwa katika kikao baraza kinachodili mambo mbalimbali ikiwemo haki na wajibu katika Utumishi wa Umma na maslahi ya wafanyakazi.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka MNH-Mloganzila wakiwa katika kikao baraza kinachodili mambo mbalimbali ikiwemo haki na wajibu katika Utumishi wa Umma na maslahi ya wafanyakazi.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Kinywa na Meno, Dkt. Deogratias Kilasara akichangia mada katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wakati wa majadiliano.

Naibu Kaimu Mkurugenzi Mtenaji wa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila, Dkt Julieth Magandi akiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi ambapo Dkt. Magandi ni mjumbe wa kikao hicho.

Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka MNH-Mloganzila akichangia mada wakati majadiliano baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila , Prof. Lawrence Mseru akiongoza kikao cha Baraza la wafanyakazi MNH -Mloganzila. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Nicholous Mshana, kulia ni Katibu Msaidizi Bi. Neema Njau.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Muhimbili (Upanga & Mloganzila), Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho.


Na Dorcas David

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga & Mloganzila unakusudia kununua vifaa tiba zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wagonjwa wanaofika katika hospitali hizo kupatiwa matibabu ikiwa ni mipango yake ya kuboresha huduma za matibabu kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Muhimbili Upanga na Mloganzila, Prof. Lawrence Museru wakati akijibu maswali ya wajumbe mbalimbali wa Baraza la Wafanyakazi ambao walitaka kujua mipango ya hospitali katika kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hizo. 

Prof. Museru amesema Muhimbili Upanga & Mloganzila itaongeza mashine ya ultrasound, ECHO, ECG, fluoroscopy, CT-Scan pamoja na vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya vyumba vya upasuaji na vyumba vya kulaza wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, amesema tayari hospitali imeshatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kununua vifaa tiba pamoja na kuboresha maeneo mbalimbali ya kutoa huduma.

Akizungumzia maslahi ya wafanyakazi, Prof. Museru amesema hospitali inaendelea kuboresha na kulipa wafanyakazi wake kwa wakati ili kuongeza motisha katika utendaji kazi wao.

Awali, Wajumbe Baraza la Wafanyakazi waliomba hospitali hizo kuongeza vifaa tiba katika vyumba vya upasuaji na vyumba vya kulaza wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalimu.

Akichangia mada ya uboreshaji wa huduma za matibabu, Dkt. Moses Mulungu, Dkt. Elisha Osati na Bw. Jamiru  Japhary kwa pamoja waliomba uongozi wa hospitali kuimarisha vifaa tiba ili kukabiliana na ongezeko la wagonjwa.

Wajumbe kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Kaimu Mkurungezi wa Huduma za Tiba Shiriki, Dkt. Lulu Sakafu, Mtekinolojia Mwandamizi, Dkt. Ahamed Sauko nao walitoa angalizo la uboreshaji wa vifaa tiba mbalimbali.