Muhimbili, Dodoma RRH yatoa huduma ya afya mkutano mkuu wa CCM

Mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipatiwa huduma ya matibabu na Dkt. Ahmed Suphian wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Dkt. Nancy Urassa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (DRRH). Mkutano unafanyika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).

Baadhi ya wataalamu wa afya wakitoa huduma kwa mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).

Dkt. Nancy Urassa na Dkt. Innocensia Safari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (DRRH) wakitoa huduma ya afya kwa mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).

Dkt. Lutfi Abdalla wa Muhimbili akitoa huduma katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mtaalamu wa maabara, Bi. Janeth Julius akitoa huduma kwa mgonjwa aliyefika katika Banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (DRRH) kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu.

Wataalamu wa afya wakiendelea kutoa huduma katika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).


Na John Stephen

Wajumbe mbalimbali wamefika katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupatiwa huduma ya magonjwa ya dharura, kupima kiwango cha sukari mwilini, kupima presha pamoja na huduma nyingine.

Huduma ya matibabu inayotolewa na wataalamu wa Muhimbili kwa kushirikiana na wenzao wa Dodoma RRH katika Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC).