Muhimbili kuendelea kutambua Mchango wa Madaktari

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru , akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU) Tawi la Muhimbili

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU) Tawi la Muhimbili Dkt. Siril Harya, akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU) ngazi ya taifa Dkt. Samwel Rweyemamu akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.

Mwakilishi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt. Lilian Mnabwiru akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU) tawi la Muhimbili

Madaktari wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya MNH.

Madaktari wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya MNH.

Madaktari wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya MNH.

Madaktari wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya MNH.

Madaktari wakifuatilia mkutano


Na Sophia Mtakasimba

Hospitali ya Taifa Muhimbili inatambua mchango mkubwa sana unaotolewa na madaktari katika maboresho ya sekta ya afya hususani uanzishwaji wa huduma za kibingwa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru  wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU) tawi la Muhimbili .

“Madaktari wana umuhimu wa kipekee, hakuna jambo linaweza kufanyika bila madaktari, mwaka 2015 wakati nafika Muhimbili kundi la kwanza kukutana nalo lilikuwa ni la madaktari bingwa  na kwa pamoja tulikubaliana tuwe na umiliki (ownership) wa hospitali hii, jambo ambalo  walilitii  na sasa tunashuhudia maboresho makubwa ya huduma hapa Muhimbili”, amesema Prof. Museru 

Prof. Museru amewataka Madaktari kwa umoja wao kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ili kudumisha mshikamano na kuwa na jukwaa la kusemea changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Nimesikia changamoto nyingi ambazo madaktari mnazipitia, naomba  mfahamu kuwa uongozi unazitambua na tayari umeanza kuzifanyia kazi na lengo letu ni kuzitatua kabisa", Amesema Prof. Museru 

Awali katika hotuba yake Mwenyekiti wa TMDPWU  tawi la Muhimbili Dkt. Siril Harya alisema kuwa zipo changamoto nyingi zinazowakabili madaktari ikiwemo kucheleweshewa malipo yao ya kuitwa na  Bima lakini pia ucheleweshwaji katika kupandishwa madaraja ya kiutumishi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TMDPWU Taifa Dkt.  Samwel Rweyemamu ameushukuru uongozi wa MNH kwa kuwezesha chama hicho tawi la Muhimbili kuwa na ofisi ambayo pia inatumika kufanya kazi za chama kitaifa.