MNH yashiriki Maonyesho katika kongamano la biashara

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni baada ya kupata maelezo kuhusu huduma za MNH,katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda linalofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa JNICC.

Mshiriki wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda akipata maelezo kuhusu maboresho na huduma mpya zinazotolewa MNH.

Mshiriki wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda akipata maelezo kuhusu maboresho na huduma mpya zinazotolewa MNH.

Na Sophia Mtakasimba

Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) imeshiriki maonyesho katika Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda, maonyesho hayo yanafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar Es Salaam.