Mloganzila kuendelea kuimarisha usalama wa watoa huduma mahala pa kazi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Sis. Redemptha Matindi akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyolenga kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa ambukizi mahala mpa kazi.

Baadhi ya washirki wa mafunzo hayo wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.

Mkuu wa Idara ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Mwanaidi Msuya akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washirki wa mafunzo hayo wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.


Na Dorcas David

Wataalamu wa afya Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wamepatiwa mafunzo ya namna bora ya kuzuia na kujikinga na magonjwa ambukizi mahala pa kazi.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tano yamedhaminiwa na Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushikiana na shirika linalojihusisha na kuboresha huduma za afya kutoka Ujerumani (GIZ). 

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uuguzi na Ukunga MNH-Mloganzila Sis. Redemptha Matindi amesema hospitali imekuwa ikizingatia usalama wa watumishi mahala pa kazi kwa kuhakikisha miundombinu na vifaa tiba vinatumika kwa kufuata ushauri wa wataalam.

 “Hospitali imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya mara kwa mara ikiwemo ya kujikinga na maambukizi wakati wa kutoa huduma kupitia Kitengo cha Huduma Bora kwa Mteja kwa kuzingatia miongozo na sera za Wizara ya Afya kwa lengo la kupambana na kuzuia maambukizi” amesema Sis. Matindi.

“Sambamba na mafunzo haya uongozi pia umekuwa ukitoa vitendea kazi vya kujikinga na maambukizi kwa watumishi wawapo kazini wakati wa kutoa huduma ikiwa ni takwa la kisheria la kuhakikisha usalama mahala pa kazi” ameongeza Sis. Matindi.

Pamoja na hayo amesema kuwa uongozi umeweka vifaa vya kuzuia majanga mbalimbali ikiwemo ya moto kwa kuweka mifumo ya kuhisi moshi kama kiashiria cha moto endapo utatokea, vifaa vya kumwaga maji (sprinklers) na alam pale moto unapotokea sehemu ya kutolea huduma.

Katika mafunzo hayo wataalamu walioshiriki mafunzo wametakiwa kuchukua hatua madhubuti kwa kusimamia kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kujilinda na kumlinda mteja na kufanya hospitali kuwa mahala salama pa kutolea huduma bora.