Mafunzo ya Huduma bora kwa wateja Muhimbili yaendelea kwa watumishi wa jengo la Maternity
Mkuu wa kitengo cha Mafunzo na Utafiti Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga , akitoa mada wakati wa mafunzo ya huduma bora kwa wateja.
Mtoa mada Bi. Sophia Sanga akizungumza wakati wa mafunzo ya huduma bora kwa wateja.
Mtoa mada Bi. Martha Edward akizungumza wakati wa mafunzo ya huduma bora kwa wateja.
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Na Sophia Mtakasimba & Angela Mndolwa
Mafunzo ya huduma bora kwa wateja yanayoendeshwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili yameendelea katika siku ya tatu , ambapo leo ilikuwa ni zamu ya watumishi wa jengo la maternity ambao ni Madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya , maafisa ustawi wa jamii, wahasibu pamoja na wafamasia.