Mabalozi wa Oman, Kuwait, Saudia Arabia, Palestina, Morocco na Misri watembelea Muhimbili

Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai, Balozi wa Palestina Mh. Hamdi Abu Ali, Mkurugenzi wa Shirika la Albasam Prof. Emadi Bukhari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge, Balozi wa Saudi Arabia Mh. Mohamed Bin Mansour Almalik, Balozi wa Kuwait Mh. Mubarak Alsehaijan, Balozi wa Oman Mh. Ally Abdallah Almahruqi na Balozi wa Misri Mh. Mohamed Gaber Abulwafa.

Mwenyekiti wa Shirika la Albasas International Prof. Prof. Emadi Bukhari akifafanua jambo kwa mabalozi waliotembelea MNH leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akifafanua jambo kwa mabalozi, kushoto ni balozi wa Saudi Arabia Mh. Mohamed Bin Mansour Almalik na kulia ni Balozi wa Morocco Mh. Abdelillah Almahruqi.

Mabalozi wakiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari


Na Sophia Mtakasimba

Mabalozi wa nchi za Saudi Arabia, Misri, Palestina, Kuwait, Morocco na Oman wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako kunafanyika upasuaji wa kurekebisha viungo (Re-Constructive surgery). Upasuaji huu unafanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa MNH na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka nchini Saudi Arabia.