Likizo ni haki ya kila mtumishi na anapaswa kuchukua kama ilivyokusudiwa.

Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu na Utawala Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Bi. Njoikiki Mapunda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamanao lililolenga kuelezea haki ya likizo kwa mtumishi aliyeajiriwa na wajibu wa mwajiri kwa mtumishi wakati wa likizo.

Baadhi ya watumishi waliohudhuria kongamano hilo wakisikiliza kwa makini mada zinazowasilishwa katika kongamano hilo

Afisa Utumishi Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Bw. Julius Kiduli akitoa mada wakati wa kongamano lililolenga kuelezea aina za likizo ambazo mtumishi anapaswa kuchukua kwa mwaka.

Afisa Utumishi MNH-Mloganzila Bi. Consolatha Assenga akiwasilisha mada katika kongamano hilo lilifanyika hospitalini hapo.

Baadhi ya watumishi waliohudhuria kongamano hilo wakisikiliza kwa makini mada zinazowasilishwa katika kongamano hilo.


Na Dorcas David

Watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wametakiwa kutambua kuwa likizo ni haki ya kila mtumishi na sio kitu anachopewa mtumishi kama upendeleo.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Utumishi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Bw. Julias Kiduli katika  kongamano lililolenga kuelezea haki za likizo kwa mtumishi na wajibu wa muajiri kwa mtumishi katika kumpatia stahiki zake za likizo.

 Bw. Kiduli amesema kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa likizo ni haki yake ya msingi na anapaswa kuchukua mara moja kwa mwaka ili aweze kupata muda wa kupumzika na baadaye kurejea kwenye majukumu yake kama kawaida.

 “Ni wajibu wa kila mtumishi kuchukua likizo yake ya mwaka kama inavyotakiwa kwani hii ni haki yake hivyo lazima uchukue bila kipingamizi chochote” amesema Bw. Kiduli.

“Endapo muajiri ataona kuwa kuna haja ya wewe kuwepo kwa kipindi ambacho unataka kuchukua likizo yako, anapaswa kuomba na kama utaridhia basi mtakubaliana  namna gani anaweza kufidia likizo yako  kwa wakati huo” 

Kwa upande wake Afisa Utumishi MNH-Mloganzila Bi. Consolatha Assenga amesema kuwa wameamua kutoa elimu hiyo kwa ili kupunguza malalamiko kwa watumishi na pia waweze kutambua aina za likizo ambazo wanazostahili, wajibu na stahiki wanazotakiwa kupata wakati wa likizo.

“Watumishi wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu likizo na wengine hawajui stahiki zao ambazo wanapaswa kuzipata wakati wa likizo na hii ni kutokana watumishi  kukosa elimu kuhusu aina za likizo wanzostahili kupata”amesema Bi. Assenga.

Kongamano hilo liliondeshwa katika Ukumbi wa Mikutano Mloganzila limehusisha wataalamu wa afya kutoka kada mbalimbali za afya hospitalini hapo.