Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lafanya usafi Muhimbili

Baadhi ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Kituo cha Ilala jijini Dar es Salaam wakifanya usafi nje ya jengo la Mwaisela ktika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya utumishi wa umma ambayo yalianza Juni 16-23, 2020. Askari hao wamefanya usafi katika Jengo la Mwaisela, Kibasila, Sewahaji, Jengo la Wazazi pamoja na maeneo mengine.

Baadhi ya askari wa Zimamoto na Uokoaji kutoka Kituo cha Ilala jijini Dar es Salaam wakiendelea na usafi wa mazingira katika Jengo la Wazazi lilipo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Askari wa Zimamoto na Uokoaji kutoka Kituo cha Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Muhimbili. Katikati ni mmoja wa watumishi wa Muhimbili.


Na John Stephen

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji