Baraza la wafanyakazi latoa matokeo chanya kwa watumishi

Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila), Prof. Lawrence Museru akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyazi kinachojumuisha wafanyakazi wa MNH-Mloganzila na Upanga.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi MNH-Upanga na Mloganzila wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa katika kikao hicho.

Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya kina Mama, Dkt Nathanael Mtinangi wa MNH- Upanga akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura, Dkt. Catherine Shari kutoka MNH-Mloganzila akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi MNH-Upanga na Mloganzila wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa katika kikao hicho.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi MNH-Upanga na Mloganzila wakiwa katika kikao hicho.

Mtaalamu wa Usingizi, David Siame kutoka MNH-Upanga akichangia mada katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi mapema leo.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi MNH-Upanga na Mloganzila wakiwa katika kikao hicho.


Na Priscus Silayo

Baraza la wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) limetoa majawabu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi pamoja na kuongeza ari katika utendaji kazi. 

Kupatikana kwa majawabu hayo kutasaidia watumishi kufanya kazi kwa bidi na kuendelea kutoa huduma bora kwa ari na weledi mkubwa.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Muhimbili (Upanga &Mloganzila), Prof. Lawrence Museru amesema uongozi wa hospitali umekuwa ukitatua changamoto mbalimbali za watumishi kadiri zinavyojitokeza huku lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wagonjwa wanapatiwa huduma bora za matibabu. 

Prof. Museru amesema maslahi ya watumishi yameboreshwa ikiwemo kupitia na kuhuisha muundo wa utumishi ili uweze kuendana na hali na matarajiio ya watumishi kwa sasa.

Amesema kuwa majadiliano kuhusu changamoto na mapungufu katika sehemu za kazi, yamesaidia kuimarisha utendaji kazi na kuleta mtazamo kwa watu mbalimbali wakiwamo wagonjwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Bi. Redemta Matindi amesema katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wajumbe wamekukumbushwa kuhusu wajibu na haki katika sehemu za kazi.

“ Vikao vya baraza la wafanyakazi, vinatuleta pamoja ili kujadili changamoto zetu, pia kupitia vikao hivi tunajadili namna ya kuboresha zaidi huduma za afya pamoja na kuondoa wasiwasi kuhusu maslahi yetu,” amesema Bi. Matindi.

Baraza la Wafanyakazi, limefanyika kwa siku mbili, huku mada mbalimbali zikijadiliwa ikiwamo wajibu na haki kwa watumishi, Tughe kujenga mahusiano mahala pa kazi na muundo mpya wa watumishi.