Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, imempatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu kutumia mashine ya oxygen muda wote ili aweze kupumua.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza idadi ya vitanda katika wodi za wagonjwa wanaohitaji huduma za uangalizi maalum (ICU) kutoka 25 hadi 78 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa hospitali wa kuboresha miundombinu ya kutoa hudum ...
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa vya kuhifadhia taka kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Msaada wa vifaa hivi una thamani ya Tshs. 5,000,000 ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi kwa ...
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kufanya upandikizaji wa ULOTO (bone marrow transplant) mwishoni mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi na kugharimu fedha nyingi. ...
Mtoto Hillary Plasidius mwenye umri wa miaka 8 aliyelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila kwa muda wa miezi minane na wiki mbili aruhusiwa huku hospitali ikimsamehe gharama za matibabu na kumpatia msaada wa wheelchair.< ...
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya zoezi la uchunguzi wa macho bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya saratani ya jicho kwa watoto (Retinoblastoma).